Saturday, May 12, 2012

SI TUBONGE TU(part 2)


Wangapi wenu mnabonga kuhusu Malaya
Na wangapi wenu pesa zenu
Zi kwenye vibeti vya Malaya
But still nikitaja hili jina
Napata macho yaliyokodolewa
Ni-ka nabonga kikamba nikiwa New York city, HAMNINYITI
Si mnanielewa
Mi nabonga kuhusu visa vilivyo nasi
Visa vya enzi za mababu
Na mababu wa mababu zetu
Bali hadi sasa havijaongelewa kwa kina
Mbona unajua kijana aliyelazimishwa na mamaye
Kumpandilia,
Na baada ya kisa cha kwanza
Ikakuwa ndiwo mtindo
Ju angekataa, mamake angemweleza bwanake
Kuwa mwanaye alimbaka
Na sote tungebaki tumeshangaa
Mbona ulinyamaza?
Na mbona nilinyamaza baadaya
Na yangu maskio kushuhudia
Kijana akivunjwa nyuma
Kugeuzwa dada na kaka mwenziye
Na usiku kucha akabaki akilia
Kamasi nyepesi akilivuta
Fwanana na mwana mchanga
Mbona nilinyamaza?
Visa vingi tumeshuhudia
Bali tumebaki tumenyamaza, ju imekuwa
Ni kama ipo sheria inayosema
Tukinena kuvhusu ni taboo
Bali mi naona tukikimya ni taabu tu
Ndiyo maan sasa nabonga
Wewe ukitaka kimya
Sawa tu!
Bali kimya change nimevunja
JU  NIMEBONGA NA NITAZIDI!!

No comments:

Post a Comment