Saturday, May 12, 2012

SI TUBONGE TU (part 1)


Hakuna aliyenifunza kuvuta kaya
Hakuna atakayenisimamisha kuvuta kaya
Sijasema nimewai vuta kaya
Na bado sija kana kuwaivuta kaya
Hapana!
Maneno nakupa in swa,  haswa
Ndiyo uweze shikanisha nachosema, haswa
Naongelea visa familiar
Si lazma ziwe za yenu familia, bali
Labda mlitazama kifamilia
Kupitia habari za saa tatu, kwa runinga
Visa vya nyanya kubakwa na mjukuu
Wengine wakacheka, wengi nao wakanyamaza
Wakitingisha vichwa
Ni same trend kwa kila kisa
Kinachopokea vichwa vya habari
Name sitakimya tena
Mi nataka bonga
Hadi point mtawika nimedunga point
Mnisambazie hizo mabonga point
Ubaya ni,
Nasema tubonge
Mnanitazama maskio mmetega
Maneno mwapokea
Maana mnapata
Bali mnakimya tu
WATU, SI TUBONGE TU!!

No comments:

Post a Comment