kando ya barabara
utawapta; ata mchana
wasichana, kama wamejipanga
ready kugawa
ama utawaachia mkwanja
napenda kuongelea malaya
sabu nyi mlinyamaza
na watoi mkawapanga, yani mkawadanganya
na walipotembea, na wao walipatana
na kwenye uwanja wakajibwaga
bila kujipanga, bila rubber
na sai ndio mana tuko hapa, kwa matanga
tunachanga changa
ndio angalau tumrudishe mwanetu kwa mchanga
lakini mimi bado nawika alituwacha akiwa mchanga
na tusinge wadanganya
angalau wangekuwa wajanja
ndipo nipatapo nafasi ka hii,
nakupa kinaga ubaga
yani hakikisha akichora saba
mkononi una rubber
na iwe ni poa, date mbali na ya ku expire
na hata kidogo haina rapture
ndiyo hiyo opportunity uwe ume ii capture
No comments:
Post a Comment